Thursday, May 29, 2014

Renamo yatoa indhari kwa serikali ya Msumbiji

Renamo yatoa indhari kwa  serikali ya Msumbiji
Chama cha Upinzani cha Renamo nchini Msimbiji kimetahadharisha kuwa, nchi hiyo inaweza kutumbukia  kwenye hatari ya kutokea vita vikubwa iwapo majeshi ya  serikali ya Maputo yataendelea kuusogelea mlima Gorongosa ambao ni maficho na ngome ya  Afonso Dhlakama kiongozi wa chama hicho cha upinzani.
Taarifa iliyotolewa na Chama cha Renamo inadai kuwa, majeshi ya serikali hivi sasa yanaelekea upande wa mlima Gorongosa  ulioko katikati mwa nchi hiyo kwa lengo la kushambulia maficho ya kiongozi wa chama hicho. Kabla ya hapo, Dhlakama aliitaka serikali ya Msimbiji kuandaa mazingira mazuri yatakayokiwezesha chama chake kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali na kufanya kampeni kwa uhuru kamili kwenye maeneo tofauti nchini humo. Uchaguzi wa rais nchini Msumbiji umepangwa kufanyika tarehe 15 Oktoba mwaka huu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Chama cha Renamo kilikubali kutia saini makubaliano ya amani na chama tawala cha Frelimo mwaka 1992 baada ya kupita miaka 16 ya mapigano ya ndani, lakini baadaye Dhlakama alidai kwamba, serikali imekuwa ikikiuka makubaliano hayo ya amani  na kusababisha kujitokeza machafuko ya mara kwa mara.

Wednesday, May 28, 2014

Olusegun Obasanjo kuzungumza na Boko Haram

Olusegun Obasanjo Olusegun Obasanjo
Olusegun Obasanjo Rais wa zamani wa Nigeria ameanza juhudi za kufanya mazungumzo na shakhsia walio karibu na kundi la Boko Haram kwa lengo la  kuwakomboa wanafunzi wasichana wanaoshikiliwa mateka na kundi  hilo kwa zaidi ya siku arubaini  sasa. Vyombo vya habari vimetangaza leo kuwa, Obasanjo ameanzisha juhudi hizo ili kuzuia kufanyika operesheni za kijeshi ambazo huenda zikahatarisha maisha ya wanafunzi hao. Rais mstaafu wa Nigeria ameingiwa na wasiwasi na uamuzi wa serikali ya Abuja wa kuomba msaada kutoka madola ya kigeni katika operesheni ya kutaka kuwaokoa wanafunzi hao waliokamatwa mateka tokea mwezi uliopita. Wakati huohuo, duru za habari kutoka Nigeria zimeripoti kuwa, mmoja kati ya wanafunzi hao waliokamatwa mateka amefanikiwa kutoroka mikononi mwa wanamgambo wa Boko Haram na kusema kwamba, kati ya wanafunzi 280 wa shule ya Chibok waliokamatwa mateka, 50 kati yao walifanikiwa kutoroka. Hivi karibuni, Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran alilaani misimamo ya kundi lenye misimamo mikali la Boko Haram na kusisitiza kwamba, lengo la kundi hilo ni kuchafua taswira nzuri ya dini tukufu ya Kiislamu na kuyapatia mwanya madola ya kigeni kuingilia masuala ya ndani ya Nigeria.

Zaidi ya 60 wauawa katika miripuko ya mabomu Iraq

Zaidi ya 60 wauawa katika miripuko ya mabomu Iraq
Zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kutokea miripuko kadhaa ya mabomu nchini Iraq. Miripuko miwili ya kutegwa garini imetokea katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Mosul ambapo makumi ya watu wameuawa wakiwemo askari na wahudumu wa afya.
Halikadhalika miripuko kadhaa imelenga mji wa Tuz Khurmatu na kuuawa watu watano, wanne wakiwa wa familia moja.  Mripuko mwingine umetokea karibu na eneo la Kadhimiyah mjini Baghdad ambapo watu 16 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa.
Iraq imekuwa ikishuhudia wimbi la machafuko katika miaka ya hivi karibuni. Maafisa wa nchi hiyo wanasema kuwa, zaidi ya watu 1,000 wengi wao wakiwa raia wameuawa na wengine 1,400 kujeruhiwa katika machafuko yaliyojiri nchini humo mwezi uliopita wa Aprili.

Obama kuyapa misaada zaidi makundi ya kigaidi Syria

Obama kuyapa misaada zaidi makundi ya kigaidi Syria
Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa ataongeza misaada ya nchi yake kwa makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za kigeni kufanya mauaji dhidi ya maafisa wa serikali na wananchi Syria. Obama amesema hayo wakati aliopokuwa anahutubia chuo cha kijeshi cha Marekani huko New York. Amesema, atashirikiana na baraza la Congress la nchi hiyo kuongeza misaada kwa wanamgambo wa Syria.
Obama amesema hayo huku kukiripotiwa kuwa Washington ina mpango wa kuanza kuwapatia mafunzo ya kijeshi kwa siri wanamgambo hao katika kituo kimja cha kijeshi nchini Qatar kwa lengo la kwenda kuwashambulia askari wa serikali ya Syria. Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa na Jarida la Wall Street Journal siku ya Jumanne, wanajeshi wa Marekani wana mpango wa kuwapa mafunzo wanamgambo wanaopigana dhidi ya serikali ya Damascus wanaojiita 'Jeshi la Ukombozi wa Syria.'

Jenerali Haftar aanza tena mashambulizi Benghazi

Jenerali Haftar aanza tena mashambulizi Benghazi
Jenerali wa zamani wa jeshi la Libya Khalifa Haftar ameanza tena mashambulizi ya anga dhidi ya mji wa Benghazi ambayo yamezilenga kambi za wanamgambo kwenye mji huo.
Imeripotiwa kuwa mashambulizi hayo yameratibiwa na kufanywa na askari watiifu kwa jenerali huyo walioasi jeshini.
Haftar alianza kuwashambulia wanamgambo katika mji huo wa Mashariki mwa Libya Mei 15 akisema kuwa, anataka kuwasambaratisha na kuimarisha usalama wa nchi hiyo.
Wakati huo huo watu wenye silaha wameshambulia kikosi cha Wizara ya Mambo ya Ndani kilichopewa jukumu la kulinda serikali ya nchi hiyo. Bunge limelaani shambulizi hilo na kusema kuwa jambo hilo halikubaliki.

Hamas yawaonya Wazayuni kuhusu msikiti wa al Aqsa

Hamas yawaonya Wazayuni kuhusu msikiti wa al Aqsa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewaonya Wazayuni wasiendelee kufanya uchokozi na uharibifu katika msikiti wa al Aqsa. Izzat al Rashaq mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo sambamba na kulaani hatua ya Israel katika kujenga hekalu la Mayahudi karibu na msikiti mtukufu wa al Aqsa huko katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu amesema kuwa, njama za Israel za kujenga hekalu hilo hazipaswi kuwa sababu ya kufutwa athari za Kiislamu.
Al Rashaq ameongeza kuwa, njama za kila uchao za utawala wa Kizayuni za kujenga mahekalu ya kila aina pambizoni mwa msikiti wa al Aqsa, zinaonesha woga na kuchanganyikiwa utawala huo wakati inapogundua kuwa kila unachokifanya kinazidi kuthibitisha madai yake ya uongo kuhusiana na mji mtakatifu wa Baytul Muqddas.
Wakati huo huo Waziri wa waqfu na masuala ya kidini wa serikali halali ya Palestina huko Gaza pia amelaani njama za Israel dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuwa, lengo la Tel Aviv la kujenga hekalu ya Kiyahudi katika umbali wa mita 200 tu magharibi mwa msikiti mtukufu wa al Aqsa ni njama za kutaka kubadilisha muundo wa Kiislamu na Kiarabu wa mji wa Quds wenye kibla cha kwanza cha Waislamu