Wadau, kama tunavyojua Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekiel Wenje aliwasilisha Maoni ya Kambi ya Upinzani. Miongoni mwa hoja alizozitoa Wenje jana ni kuishutumu Tanzania kuingilia mambo ya ndani ya Rwanda na kuilalamikia Tanzania kwa kitendo chake cha kupeleka majeshi nchini DRC kuwaondoa waasi wa M23, hotuba ambayo imelalamikiwa na kulaaniwa kila kona ya nchi hii na nje ya nchi. Baada ya hotuba hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe aliongea kwa ukali na kuwatahadhalisha Watanzania kutokana na uchochezi unaofanywa na Wenje. Pia Membe alilaani kitendo cha Wenje kuwa msemaji wa Serikali ya Rwanda ndani ya Bunge la Tanzania hali ambayo ameiita ni usaliti mkubwa.
Tumesikia pia utetezi wa Mwenyekiti wa CHADEMA na UKAWA, FREEMAN MBOWE akisema kuwa alichowasilisha Wenje ni Maoni ya Kambi ya Upinzani na kwa hali hiyo yalipata baraka kutoka kwa viongozi wa Kambi hiyo. Baada ya majibu hayo ya Mbowe, nilitegemea kuwa kama kawaida yao wataweka hotuba hiyo kwenye Mtandao wao wa www.chademablog.blogspot.com. Hata hivyo, mpaka sasa hawajaweka hotuba hiyo huku wananchi wengi wakitaabika kuitafuta bila ya mafanikio. Kutokana na hali hiyo nimelazimika kuwauliza CHADEMA, kama mnasema kuwa alichowasilisha Wenje ni maoni ya Upinzani, mbona mnagwaya kuyaweka kwenye mtandao wenu?
No comments:
Post a Comment