Tuesday, May 27, 2014

Aibu Mpya Elimu-Vitabu vya SHIGONGO vyaingizwa katika mitaala ya shule!


Hii sasa wadau ni full majanga! eti vitabu vya yule jamaa wa udaku eti vimeingizwa katika mitaala ili kufundishia watoto wetu!

hivi waziri wa elimu yuko likizo au? Hii kwa kweli ni bora tuandamane nchi nzima

--------------------------------




Srori: Richard Bukos
Kwa miaka mingi wanafunzi wa hapa nchini wamekuwa wakitumia vitabu vya watunzi mbalimbali ulimwenguni kama vile, The river between, Song of Lawino na vinginevyo hatimaye Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika, IST) imekiingiza kwenye mtaala wake wa kiswahili, kitabu cha mtunzi mahiri wa riwaya hapa nchini, Eric James Shigongo kiitwacho kifo ni haki yangu.

Akizungumza na gazeti hili shuleni hapo hivi karibuni, Mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Madam Hilda, alisema shule yake imeamua kutumia kitabu hicho kwenye mtaala wake baada ya kamati ya shule hiyo kukipitia kiundani na kubaini ubora wa hadithi zake zinazokwenda na wakati tuliopo pamoja na matumizi sanifu ya lugha ikiwemo mambo mengi ya kujifunza.

Hilda alisema baada ya kuona umuhimu uliopo kwenye kitabu hicho shuleni hapo shule iliamua kumuita mtunzi huyo ambaye walimu na wanafunzi walikuwa na shauku ya kumuona ‘live’ badala ya kusoma riwaya zake kwenye vitabu.
Kufuatia wito huo, Shigongo alifika chuoni hapo na kukutana na wanafunzi wa shule hiyo ambao walimuuliza maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiwatatiza kwenye riwaya.

Wanafunzio hao walimuomba Shigongo awafundishe mambo kadhaa kwenye utunzi wa riwaya ambapo walionekana kuyafurahia majibu waliyopewa ambayo yalionekana kuwaingia vyema akilini.

Baada ya kuwafundisha mambo mbalimbali wanafunzi hao walimshukuru Shigongo kwa kuwapa baraka za kutumia kitabu chake kwenye masomo yao na kuwapa fursa ya kuwapa ushauri muda wowote ambao watauhitaji.

Kufuatia wanafunzi hao kutumia kitabu hicho mitihani mbalimbali ya wanafunzi hao ikitoka kwenye kitabu hicho hivyo wanafunzi hao wanatakiwa kukichimba zaidi kitabu hicho.

Mbali na riwanya hiyo Shigongo aliwatafadhalisha wanafunzi hao kutobweteka na kutumia nguvu za wazazi wao kwani hawajui ya kesho na keshokutwa.

Aliwashauri wanafunzi hao kutokuwa kama wazazi wao kimaisha na kuwa zaidi ya wazazi wao yaani kama baba alikuwa mkuu wa wilaya mtoto anatakiwa kuwa waziri na kama baba alijenga ghorofa moja mtoto anatakiwa kuwa zaidi.
JF

No comments:

Post a Comment