Wednesday, May 28, 2014

Al Sisi aongoza katika uchaguzi wa rais wa Misri



Al Sisi aongoza katika uchaguzi wa rais wa Misri
Baada ya kuhesabiwa kura za baadhi ya majimbo, matokeo yanaonesha kuwa mkuu wa jeshi wa zamani wa Misri Abdul Fattah al Sisi anaongoza katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo. Vyombo vya habari vya Misri vimeripoti kuwa al Sisi anaongoza kwa asilimia 93 ya kura akimuacha mbali mgombea wa mrengo wa kushoto Hamdeen Sabbahi.
Hata hivyo matokeo hayo si jambo la kustaajabisha katika uchaguzi huo ambao ulisusiwa na makundi mengi ya Misri, huku waliojitokeza kupiga kura wakiwa ni watu wachache sana hadi kuilazimisha serikali inayoungwa mkono na jeshi kuongeza siku zaidi ya uchaguzi kwa tamaa kwamba huenda watu wakajitokeza.
Hata baada ya hatua hiyo, duru za mahakama ya Misri zimeripoti kuwa, watu walijitokeza kwa asilimia 44.4 katika uchaguzi huo unaoonekana kuwa umefanyika ili kuhalalisha mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa dhidi ya rais halali iliyechaguliwa na wananchi, Muhammad Mursi.

No comments:

Post a Comment