Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametaka amani na utulivu urejeshwa nchini Libya. Kwa mujibu wa msemaji wake Stephane Dujarric, Ban Ki Moon ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na hali ya hivi sasa nchini Libya hasa kuongezeka harakati za kijeshi katika mji mkuu Tripoli na pambizoni mwake. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa, mapigano ya kijeshi yanaweza kuharibu kujitolea kulikofanywa na raia wa Libya katika kipindi cha mapambano yao ya kujikomboa na kupata hadhi hasa wakati huu muhimu wa mwenendo wa mpito wa kisiasa. Aidha amesema kuwa, Ban Ki Moon amezitaka pande zote za Libya kuanza mazungumzo na kujiepusha na kuchukua hatua zitakazotilia shaka na kudhoofisha ubadilishanaji madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini humo.
Licha ya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na machafuko huku mgogoro wa kisiasa ukishadidi nchini humo, imepangwa kuwa uchaguzi wa Bunge la Libya utafanyika Juni 25.
No comments:
Post a Comment