Tuesday, May 27, 2014

Maafisa wa Somalia wanunia Kenya

 

Wakimbizi wa Somali wanaoshi kambini Dadaab
Maafisa wa Somalia wamekataa kukutana na maafisa wa serikali ya Kenya na maafisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, ili kujadili mkataba uliofikiwa mwaka jana kuhusu kuwarejesha kwao wakimbizi wasomali wanaoishi nchini humo.
Barua kutoka kwa waziri wa mambo ya nje wa Somalia, ambayo BBC imeweza kuiona, inasema kuwa shughuli inayoendelea ya kuwazuilia wakimbizi na kuwarejesha baadhi kwa nguvu Somalia, inakiuka makubaliano hayo.
Shirika la wakimbizi la Human Rights Watch linasema kuwa tangu mwezi jana maafisa wa Kenya wamekuwa wakiwakamata na kuwatesa wakimbizi wasomali na kuwarejesha baadhi yao kwa nguvu katika kambi za wakimbizi Kaskazini mwa Kenya.

No comments:

Post a Comment