Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewaonya Wazayuni wasiendelee kufanya uchokozi na uharibifu katika msikiti wa al Aqsa. Izzat al Rashaq mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo sambamba na kulaani hatua ya Israel katika kujenga hekalu la Mayahudi karibu na msikiti mtukufu wa al Aqsa huko katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu amesema kuwa, njama za Israel za kujenga hekalu hilo hazipaswi kuwa sababu ya kufutwa athari za Kiislamu.
Al Rashaq ameongeza kuwa, njama za kila uchao za utawala wa Kizayuni za kujenga mahekalu ya kila aina pambizoni mwa msikiti wa al Aqsa, zinaonesha woga na kuchanganyikiwa utawala huo wakati inapogundua kuwa kila unachokifanya kinazidi kuthibitisha madai yake ya uongo kuhusiana na mji mtakatifu wa Baytul Muqddas.
Wakati huo huo Waziri wa waqfu na masuala ya kidini wa serikali halali ya Palestina huko Gaza pia amelaani njama za Israel dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuwa, lengo la Tel Aviv la kujenga hekalu ya Kiyahudi katika umbali wa mita 200 tu magharibi mwa msikiti mtukufu wa al Aqsa ni njama za kutaka kubadilisha muundo wa Kiislamu na Kiarabu wa mji wa Quds wenye kibla cha kwanza cha Waislamu
No comments:
Post a Comment