Maafisa wa Bahraina wamemuachilia huru mwanaharakati mashuhuri wa kutetea haki za binadamu aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa ajili ya kuhusika katika maandamano ya kupinga serikali. Nabeel Rajan mwanzislishi wa Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain alifungwa mwaka 2012 kwa madai ya kuratibu na kushiriki maandamano dhidi ya utawala wa Aal Khalifa. Baada ya kuachiliwa huru mkuu huyo wa Kituo Cha Haki za Binadamu cha Baharain amesisitiza kuachiliwa huru wafungwa wote wa kisiasa nchini humo.
Huko nyuma makundi ya kutetea haki za binadamu ya kieneo na kimataifa kama Amnesty Internationa na pia Human Rights Watch yaliutaka utawala wa Bahrain umwachiliwe huru Nabeel Rajab. Bahrain tangu mwaka 2112 inashuhudia maandamano ya wananchi ya kutaka mageuzi na kupinga serikali ambayo yamekuwa yakikandamizwa na vikosi vya utawala wa Manama.
No comments:
Post a Comment