Ukitaka waweza kuwaita Team Melli, Shirane Iran kwa maana ya The Iranian Lions, au The Princes of Persia, hapa nafupisha tu, …jamani wanaspoti wenzangu, haya yote ni majina ya timu ya kandanda ya taifa ya Iran, ambao wanashika nambari moja huko barani Asia kwa viwango vya ubora wa kandanda, vinavyotambuliwa na shirikisho la soka la kimataifa la dunia, Fifa,…nambari 37 duniani..
Mnamo mwaka 1978, ilikuwa ndio mara ya kwanza kwa taifa hili kucheza kwenye fainali kama hizi za kandanda za kombe la dunia, ambazo zilifanyika nchini Argentina, na wenyeji wakitwaa ubingwa wa michuano hiyo…wakishika mkia, kwa kujikusanyia pointi moja, katika kundi lililokuwa na nchi za Peru, Netherland na Scotland.
Baada ya hapo, iliwachukuwa miaka ishirini, Wairani kuishuhudia timu yao ikishiriki fainali hizo, ambazo zilifanyika nchini Ufaransa, na hiyo ilikuwa ni mnamo mwaka 1998, na pia wenyeji kuchukuwa ubingwa wa michuano hiyo..na pamoja na kuondoshwa kwenye hatua ya makundi, bado walijiandikia historia baada ya kuwafunga mahasimu wao Marekani, mabao mawili kwa moja, katika pambano la kihistoria..na wakishika nafasi ya tatu ya kundi..
Ikawachukuwa tena miaka minane, kufuzu kwa fainali nyingine za kombe hilo, ambapo ikifuzu kwa fainali zilizofanyika nchini Ujerumani, mnamo mwaka 2006, ambapo ilishika nafasi ya mwisho kwenye kundi lililokuwa na nchi za Mexico, Ureno na Angola..ikijipatia pointi moja tu.
Hata hivyo wameshiriki kwenye michuano kumi na miwili ya AFC Asian cup, mara ya kwanza ikiwa ni mnamo mwaka 1968, wakichukuwa ubingwa mwaka 1968, 1972, na mwaka 1976…
Unapoitaja Iran, basi moja kwa moja hutaacha kumzungumzia staa wake hatari Ally Daei, ambae amevunja rekodi kubwa kweli kweli nchini humo, akiwa ameichezea Iran mechi 149, na kutikisa nyavu mara 109..
Kihistoria baada ya mapinduzi ya mnamo mwaka 1979, futiboli nchini humo ikawekwa pembeni, na kipindi cha miaka ya themanini, Iran ikashindwa kushiriki michuano ya soka ya dunia, kufuatia vita baina yao na majirani zao Iraq vilivyodumu kwa miaka takriban minane…
Hakukuwa na ligi ya ndani, na wala timu ya taifa haikushiriki michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za mwaka 1982 nchini Hispania na ile ya kufuzu kwa fainali za mwaka 1986 nchini Mexico..lakini ligi ya ndani iliyojulikana kama Qods ikaanzishwa mnamo mwaka 1989..
Pamoja na kushindwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 1990 kule nchini Italia, na zile za mwaka 1994 kule nchini Marekani, bado wimbi la wnandinga wenye vipaji lilianza kuvuma nchini humo, na wakishika nafasi ya tatu kwenye michuani ya AFC Asian Cup, mnamo mwaka 1996, huku moja kati ya ushindi wa kukumbukwa ukiwa ni ule wa mabao 3-0 dhidi ya Saudi Arabia, na 6-2 dhidi ya Korea ya kusini..
Mnamo April 4 ‘2011, bosi wa zamani wa Real Madrid ya Hispania Mreno Carlos Queiroz akasaini mkataba wa miaka miwili na nusu kuifunza Iran, hadi mwisho wa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil,,
Ikaanza kampeni kwa kuishindilia Maldives 4–0 mechi ya kwanza ya duru ya pili ya kufuzu, katika ushindi wa jumla wa matano kwa sifuri, na baadae ikapangwa kwenye kundi na katika duru ya tatu, na nchi za Indonesia, Qatar na Bahrain.
Ikakaa kileleni baada ya kuibutua Bahrain 6–0 nyumbani Azadi Stadium,ikiwemo pia kumualika nyota wa zamani wa timu za taifa za vijana za Ujerumani,Ashkan Dejagah, aliyepiga bao mbili kwenye mechi dhidi ya Qatar..
Ndipo duru ya mwisho ya nne kuelekea kufuzu, wakipangwa na Korea ya kusiniQatar, Uzbekistan, na Lebanon kwenye kundi, ambapo sasa Queiroz akiwaita wachezaji wapya wanaosakata kandanda la kulipwa nje ya nchi hiyo, kama Reza Ghoochannejhad.
Iran ikafuzu kwa fainali za Brazil za mwaka huu, na sasa wapo kundi moja la F na Argentina, Nigeria, na Bosnia and Herzegovina na tiketi za mechi yao dhidi ya Argentina, zote zikiwa zimekwishauzwa…
Kati ya matukio ya kukumbukwa, ni kwenye mchezo wa kuwania kufuzu, kwa fainali za mwaka 2010, mechi dhidi ya Korea ya kusini, mnamo 17 June 2009, mjini Seoul, pale nyota wa timu hii, Javad Nekounam, Ali Karimi, Hossein Kaebi, Masoud Shojaei, Mohammad Nosrati, Vahid Hashemian, na nahodha Mehdi Mahdavikia wakivaa vitambaa vya mkononi vya rangi ya kijani, kama kusapoti chama cha upinzani Iranian Green Movement katika kipindi cha uchaguzi wa raisi wan chi hiyo mwaka huo.
Ripoti zikatoka zikisema kwamba, shirikisho la soka la Iran liliwafungia nyota hao saba, lakini Fifa ilipotaka ufafanuzi toka shirikisho hilo, wakajibiwa kwamba hakukuwa na hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yao, na baadae baadhi ya kama Javad Nekounam, Masoud Shojaei, Mehdi Mahdavikia, na Ali Karimi wakarejea kikosi cha timu ya taifa.
Tutawaona hawa jamaa…

No comments:
Post a Comment