Tuesday, May 27, 2014

Uzalishaji uchumi nchini Afrika kusini umepungua

 

Jacob ZumaJacob Zuma
Taasisi ya takwimu ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, kiwango cha uzalishaji wa uchumi katika nchi hiyo inayoongoza kwa viwanda barani Afrika, ulipungua katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzoni mwa mwaka huu wa 2014. Kwa mujibu wa taasisi hiyo, kiwango cha uchumi wa nchi hiyo kimeshuka kwa asilimia 0.6. Taasisi hiyo ya takwimu imeyasema hayo hii leo na kuongeza kuwa, kiwango cha kushuka uchumi wa ndani ni zaidi na ilivyotabiriwa na wataalamu wa masuala ya kiuchumi. Chanzo kikuu cha kuzorota uchumi nchini humo ni kupungua kwa uzalishaji wa sekta ya madini hasa kufuatia migomo ya mara kwa mara ya wafanyakazi iliyoanza tangu tarehe 23 Januari mwaka huu na hivyo kuathiri hali ya uchumi. Mbali na sekta ya madini, pia viwanda vingine havikufanya vizuri katika uzalishaji wake ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya mwanzoni mwa mwaka huu. Itakumbukwa kuwa katika sherehe za kuapishwa kwake hapo siku ya Jumamosi iliyopita mjini Pretoria, Rais Jacob Zuma  wa nchi hiyo alisema kuwa, wananchi wa Afrika Kusini watashuhudia mabadiliko ya kiuchumi katika kipindi chake hiki cha awamu ya pili, huku akiahidi kuboresha sekta za miundombinu, nishati, elimu, afya na kuwaandalia nafasi za ajira wananchi wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment