Waziri wa Mambo ya Ndani wa Niger amesema kuwa, watu 40 wanaofungamana na mrengo wa Spika la Bunge la nchi hiyo wametiwa mbaroni kwa kufanya njama za mapinduzi ya kijeshi nchini humo. Hassoumi Massoudou amesema kuwa, watu hao wametiwa mbaroni baada ya vyombo vya usalama vya nchi hiyo kufuatilia nyendo zao. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nger amesisitiza kwamba watu wote waliotiwa mbaroni ni wanachama wa ‘Harakati ya Demokrasia ya Niger’ chama kinachoongozwa na Hama Amadou Spika wa Bunge la nchi hiyo. Waziri Massaoudou amesisitiza kuwa uchunguzi bado unaendelea kuhusiana na kadhia hiyo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, watu hao wanashukiwa kuhusika katika ufyatuaji wa risasi uliofanyika siku ya Jumatatu iliyopita dhidi ya nyumba ya mbunge mmoja kutoka chama tawala na pia wanahusishwa na shambulio la miripuko dhidi ya jengo la chama tawala mjini N’Djamena.
No comments:
Post a Comment