Sunday, May 25, 2014

Wanajeshi wa Ufaransa wapigana na Waislamu CAR

 

Wanajeshi wa Ufaransa wapigana na Waislamu CAR
Kumeripotiwa mapigano makali baina ya wanajeshi wa Ufaransa na Waislamu watiifu kwa kundi la Seleka huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Walioshuhudia wanasema jana Jumamosi wanajeshi wa Ufaransa wakiwa wanapata himaya za helikopta zenye mizinga walikabiliana na wapiganaji Waislamu katika mji wa Bambari wa nchi hiyo. Ripoti zinasema helikopte za kijeshi za Ufaransa zilifyatua maroketi dhidi ya ngome za wapiganaji Waislamu mjini Bambari. Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika machafuko mwezi Machi mwaka 2013 na katika miezi ya hivi karibuni magenge ya magiadi wa Kikristo wajuliakano kama anti-Balaka wamekuwa wakiwaua kwa umati Waislamu walio wachache nchini humo. Mwezi Desemba mwaka jana Ufaransa ilivamia nchi hiyo ambayo ni koloni lake la zamani kwa kisingizio cha kuzuia mapigano. Hata hivyo wanajeshi wa Ufaransa wajulikanao kama Sangaris wamekuwa wakiwashambulia Waislamu na kupuuza ugaidi unaofanywa na wanamgambo wa Kikristo. Shirika la kutetea haki za binaadmau la Amnesty International limeonya kuwa kile kinachojiri huko  Jamhuri ya Afrika ya Kati dhidi ya raia Waislamu ni 'mauaji ya umati.' Katika wiki za hivi karibuni kumeshuhudiwa maandamano dhidi ya Ufaransa katika nchi hiyo ya Kiafrika.

No comments:

Post a Comment