Thursday, May 29, 2014

Renamo yatoa indhari kwa serikali ya Msumbiji



Renamo yatoa indhari kwa  serikali ya Msumbiji
Chama cha Upinzani cha Renamo nchini Msimbiji kimetahadharisha kuwa, nchi hiyo inaweza kutumbukia  kwenye hatari ya kutokea vita vikubwa iwapo majeshi ya  serikali ya Maputo yataendelea kuusogelea mlima Gorongosa ambao ni maficho na ngome ya  Afonso Dhlakama kiongozi wa chama hicho cha upinzani.
Taarifa iliyotolewa na Chama cha Renamo inadai kuwa, majeshi ya serikali hivi sasa yanaelekea upande wa mlima Gorongosa  ulioko katikati mwa nchi hiyo kwa lengo la kushambulia maficho ya kiongozi wa chama hicho. Kabla ya hapo, Dhlakama aliitaka serikali ya Msimbiji kuandaa mazingira mazuri yatakayokiwezesha chama chake kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali na kufanya kampeni kwa uhuru kamili kwenye maeneo tofauti nchini humo. Uchaguzi wa rais nchini Msumbiji umepangwa kufanyika tarehe 15 Oktoba mwaka huu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Chama cha Renamo kilikubali kutia saini makubaliano ya amani na chama tawala cha Frelimo mwaka 1992 baada ya kupita miaka 16 ya mapigano ya ndani, lakini baadaye Dhlakama alidai kwamba, serikali imekuwa ikikiuka makubaliano hayo ya amani  na kusababisha kujitokeza machafuko ya mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment