Ni wazi kwamba katika maisha ya mwanadamu, mara nyingi kila mtu anakuwa na mtu fulani anayemvutia kwanye mambo fulani fulani na kumfanya anayevutiwa kupenda kuiga toka kwa yule anayetenda "Role Model".Katika siasa wapo watu wa namna hii vile vile ambapo wadau na wanasiasa wanaochipukia hutamani kuwaiga!.
Binafsi kwa hapa Tanzania; Katika medani za siasa, 'Role Model' wangu ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete!. Mwanasiasa huyu amekuwa akinivutia zaidi katika jambo moja kubwa: Jinsi anavyoshughulikia migogoro ya kitaifa na kimataifa.Mh. Kikwete amekuwa anaonesha uwezo mkubwa katika kuepusha migogoro (hasa ya kisiasa), na inapotokea mgogoro umeibuka, amekuwa anaonesha umahiri mkubwa kuidhibiti kwa kutumia mbinu za kistaarabu kabisa na inapobidi kuitatua; basi amekuwa akiitatua kwa njia za kidiplomasia (mifano ni mingi mno).Kimsingi binafsi navutiwa sana na kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kutatua migogoro kwa njia ya diplomasia.Naweza kusema Rais Kikwete ndio Mwanadiplomasia bingwa wa zama hizi katika eneo letu hili la Afrika Mashariki na kati.
Awali nilidhani kwamba niko peke yangu ambaye ninamtazama Mh.Kikwete kama 'role model' lakini baadae niligundua kwamba tuko wengi.Kwa mfano Mwaka 2012 mkoani kilimanjaro, Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Mbowe alisema;
"Nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - (Freeman Aikaeli Mbowe, Nov 2012) Hii ni wazi kwamba kumbe tuko wengi tunaomuhusudu huyu Mwanasiasa!
Any way! wewe ndugu yangu sijui "Role Model" wako ni nani katika siasa za Tanzania? na kwa nini?
N.B
Kama mtu ukisoma hii mada huelewi ni bora usichangie! unaweza kusoma tu michango ya wenzako kuliko kutoa matusi humu!
No comments:
Post a Comment