Ardhi ya nyumbani: Beki wa Brazil , David Luiz ni miongoni mwa wachezaji 18 wa Chelsea wanaotarajia kushiriki kombe la dunia mwaka huu na nchi zao.
KLABU ya Chelsea ndio timu pekee ambayo wachezaji wake wengi wanaenda kushiriki fainal za kombe la dunia kuanzi mwezi ujao nchini Brazil.
Wachezaji 18 wa Chelsea wanatarajia kuzichezea nchi zao katika fainali hizo kubwa za soka duniani.
Ukiangalia vikosi vya awali vya mataifa mbalimbali na vikosi vya mwisho vya watu 23 , wachezaji wengi wa Chelsea wamechaguliwa, huku wakifuatiwa na Manchester United ambayo wachezaji wake 16 wamechaguliwa licha ya kuwa na msimu mbovu.
Kwa wenyeji Brazil, kocha Luiz Felipe Scolari amewaita Oscar, Willian, Ramires na David Luiz kuichezea nchi yao katika ardhi ya nyumbani.
Bado ana nguvu: Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard (kulia) ametajwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya England
Kama kawaida: Fernando Torres anatarajiwa kutajwa katika orodha ya mwisho ya kikosi ch Hispania licha ya kutokuwa na msimu mzuri chini ya Mourinho.
KLABU AMBAZO WACHEZAJI WAKE WENGIN WANAKWENDA KOMBE LA DUNIA
1. Chelsea (18)
2. Manchester United, Bayern Munich (16)
3. Napoli (14)
4. Barcelona, Real Madrid, Manchester City (13)
5. Juventus, Arsenal, Liverpool (12)
6. Atletico Madrid (11)
7. Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit (10)
8. Borussia Dortmund, Paris Saint-Germain (8)
9. Southampton, Schalke, Roma (7)
2. Manchester United, Bayern Munich (16)
3. Napoli (14)
4. Barcelona, Real Madrid, Manchester City (13)
5. Juventus, Arsenal, Liverpool (12)
6. Atletico Madrid (11)
7. Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit (10)
8. Borussia Dortmund, Paris Saint-Germain (8)
9. Southampton, Schalke, Roma (7)
The Blues pia wachezaji wake wawili wa England, Frank Lampard na Gary Cahill, Wawili wa Hispania, Fernando Torres na Cesar Azpilicueta na nyota wa Ubelgiji, Eden Hazard, Romelu Lukaku na Thiabaut Courtois wameitwa katika vikosi vya nchi zao.
Wachezaji wengine waliobaki watacheza kombe la dunia na nchi zao. Samuel Eto`o ataichezea Camroon, Ujerumani, Andre Schurrle, Nigeria, John Obi Mikel, Victor Moses na Kenneth Omeuro, Ghana, Christian Atsu na Uholanzi, Patrick van Aanholt.
Licha ya Man United kuvurunda zaidi msimu huu, lakini haijazuia wachezaji wake kuitwa vikosi vya timu za taifa.
Wayne Rooney, Javier Hernandez na Robin van Persie watacheza fainali za kombe la dunia, japokuwa wachezaji wawili wa klabu hiyo Tom Cleverley na Michael Carrick wote wapo katika orodha ya wachezaji wa akiba.
Amerudi kazini: Mshambuliaji wa mashetani wekundu, Robin van Persie anatarajia kuichezea Uholanzi chini ya kocha mtarajiwa wa Man United, Louis van Gaal, ambaye kwa sasa ana majukumu na timu ya taifa ya Uholanzi.
Man United imetoa wachezaji idadi sawa na mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich ambao kwa asimilia kubwa wanaunda kikosi cha Ujerumani.
Manuel Neuer, Jerome Boateng, Bastian Schweinsteiger, Toni Kross, Thomas Muller, Mario Gotze na Philipp Lahm wote wameitwa katika kikosi cha awali cha Joachim Low ambapo atachuja kupata kikosi cha mwisho cha wachezaji 23.
Miamba ya Serie A , Napoli ni klabu ya tatu ambayo wachezaji wake wengi watashiriki kombe la dunia. Wanandinga wake 14 wameitwa katika vikosi vya awali vya mataifa tofauti wakiwemo Valon Behrami, Blerim Dzemaili na Gokhan Inler
Klabu hiyo ya Italia ina wachezaji wengi kuliko miamba ya Hispania, Real Madrid na FC Barcelona, ambapo wote wana wachezaji 13 wakiwemo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Idadi hiyo ni sawa na wachezaji wa mabingwa wa sasa wa Ligi kuu soka nchini England, Manchester City wakiwemo wachezaji watatu wa Argentina, Sergio Aguero, Pablo Zabaleta na Martin Demichelis.
Arsenal na Liverpool wanaweza kuwa na wachezaji 12 nchini Brazil, ingawa Lucas Leiva anaweza kubadili idadi baada ya kuongezwa katika kikosi cha akiba cha Scolar mapema wiki hii.
Tishio: Nyota wa Barcelona, Lionel Messi ataiongoza Argentina katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mabingwa wa Italia, Juventus, wachezaji wake 12 wametajwa katika vikosi vya timu za taifa wiki hii na wanaweza kujiona hawana bahati baada ya mshambuliaji wao hatari, Carlos Tevez kutemwa na kocha Alejandro Sabella.
Vinara wa La Liga na wanafainali wa UEFA, Atletico Madrid wanafuatia kwa wachezaji wake 11 kuitwa wakiwemo watatu wa Hispania Diego Costa, Koke na Juanfran.
Klabu nyingeni ambazo wachezaji wake wengi wameitwa timu za taifa ni Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit St Petersburg (zote wachezaji), Borussia Dortmund (nane) and Southampton (saba).
Ngoma za Brazil: Nyota wa Southampton, Maya Yoshida (kulia) na wa Liverpool, Luis Suarez (kushoto) wote watacheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment